
Akizungumza na Cloudsfm.co juzi kati kwenye mgawahawa mmoja uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam, Madee anayejulikana pia kama Rais wa Manzese amefunguka kuwa toka ameanza kujihusisha na muziki hajawahi kuwa mwana hip hop na wala kuwa mfuasi wa muziki huo.
"Watu wanashindwa kutofautisha mimi siyo mwana hip hop mimi ni 'rapper' ndiyo maana naweza kuweka michano kwenye beat yeyote na nikafanya poa, nakumbuka nilipatwa na mambo mengi sana baada ya kutoa ile ngoma hip hop haiuzi sikuchukia kwa sababu nilijua kuwa waliokuwa wakinilaumu walikuwa hawajui lolote kuhusu muziki lakini walionielewa nadhani walipata picha ya kiule nilichokuwa nakaisema na kile ninachokifanya, nasiistiza mimi siyo mwana hip hop na sijawahi kuwa mfuasi wa muziki huo" alisema madee.
0 comments:
Post a Comment