ALIYOYASEMA OMMY DIMPOZ KUHUSU WALIOIKOSOA VIDEO YAKE YA ME & YOU


Haijapita wiki toka staa wa bongofleva Ommy Dimpoz alipoachia video mpya ya single ya (me & you) ft V ambapo video hiyo ilianza kupokea maoni katika kipindi kifupi tu baada ya kutoka, wengine wakiisifia na wengine wakiikosoa kwa jinsi utaalamu mbalimbali ulivyotumika ndani  ikiwemo kuonganisha picha za magorofa.
Baada ya siku kadhaa za maoni, Ommy Dimpoz aliamua kufungua kinywa chake kuzungumzia hayo maoni kwa mara ya kwanza kupitia AMPLIFAYA ya CLOUDS FM March 8 2013 saa moja usiku.
.
Namkariri akisema “Jinsi nilivyoipokea video kuna vitu niliridhika navyo na vilikuepo kwenye makubaliano lakini kuna vitu ambavyo haviko sawa katika video lakini watu wanatakiwa kufahamu mimi sina utaalamu wowote wa kuedit video, ilikua ni kazi ya Ogopa ambayo ni kampuni kubwa nilikua na imani nayo kwenye utengenezaji wa video ambayo ndio kazi yao siku zote”
“Kilichonishangaza zaidi ni kwamba mapokeo ya watu katika maoni, wanavyoiongelea ndio vitu ambavyo kidogo vimenishangaza kwa sababu mtu anatoa comment mpaka anatukana, anaponda kupita kiasi, maneno yanakua mengi kiasi kwamba unaweza kuona kama umeua vile….. unapomfikishia mtu maoni katika hali ya kujenga kuna aina ya kumwambia mtu katika hali kwamba tunajenga, huwezi kuzuia watu kuongea lakini inapofikia time inabidi watu waweze kuwa waelewa”
Kuhusu kurekebishwa kwa hiyo video, Ommy amesema bado wako kwenye mazungumzo hivyo mambo yatakaa sawa tu manake mazungumzo bado yanaendelea
.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment