
Oscar Pistorius


Reeva Steenkamp

Kesi kamili inayomkabili nyota huyo inaweza kuanza kusikilizwa miezi
kadhaa ijayo, na Pistorius nyota wa Olimpiki na Paralimpiki, ambaye hana
miguu yote miwili, anakabiliwa na hatari ya kifungo cha maisha kama
akikutwa na hatia ya mauaji
JOHNNESBURG, South Africa
MWANARIADHA nyota wa mbio za walemavu Oscar Pistorius, hatimaye leo
Ijumaa mchana ameachiwa kwa dhamana, kutokana na kesi ya mauaji ya
mpenzi wake inayomkabili.
Umauzi wa Pistorius kupewa dhamana ulitolewa na Jaji Desmond Nair, na
kuamsha furaha miongoni mwa wanafamilia wa Pistorius na mashabiki wake
ndani na nje ya Mahakama ya jijini Pretoria, huku mwenyewe akiwa
amesimama imara kama aliyenyimwa dhamana hiyo.
Kuachiwa kwa Pistorius kunafuatia wiki nzima ya usikilizaji wa maelezo
ya namna mwanariadha huyo alivyompiga risasi na kumuua mpenzi wake Reeva
Steenkamp wakiwa katika jumba lao la kifahari, asubuhi ya Siku ya
Wapendao Februari 14.
Waendesha mashtaka wamesema Pistorius, 26, anakabiliwa na kesi ya kujibu
kutokana na kupiga risasi nne kwenye mlango wa bafu ukiwa umefungwa,
huku mpenzi wake akiwa ndani. Steenkamp, 29, alikutwa na majeraha ya
risasi katika kichwa chake, mkononi na kwenye nyonga.
Upande unaomtetea Pistorius umeendelea kusisitiza kuwa mkali huyo
alimuua mkewe kimakosa, wakisema alifanya hivyo kutokana na kuhisi kuwa
amevamia na jambazi, wakataka apewe dhamana kuweza kujiandaa, kuikabili
kesi hiyo iliyoteka hisia za wengi duniani.
Kesi kamili inayomkabili nyota huyo inaweza kuanza kusikilizwa miezi
kadhaa ijayo, na Pistorius nyota wa Olimpiki na Paralimpiki, ambaye hana
miguu yote miwili, anakabiliwa na hatari ya kifungo cha maisha kama
akikutwa na hatia ya mauaji.
Dhamana hii imefungua milango ya matumaini miongoni mwa wanafamilia na
mashabiki wake, kuwa anaweza kushinda vita ya kuepuka kifungo cha
maisha.
0 comments:
Post a Comment