UMRI SAHII WA KUOA KWA MWANAUME NA KWA MWANAMKE KUOLEWA.



Mwanamke na mwanaume wawe wametimiza miaka 18 ili kufunga ndoa. Hata hivyo mwanamke anaweza kuolewa akiwa na umri wa chini ya miaka18 lakini sio chini ya miaka 15 kama atapata idhini ambayo hutolewa na baba na kama hayupo ni mama au kama wote wamefariki idhini itatolewa na mlezi wa binti huyo.

 Kama wote wamefariki basi hatahitaji idhini. Kuna wakati katika mazingira fulani mahakama inaweza kutoa idhini kwa binti kuolewa akiwa na miaka 14 lakini si chini ya hapa ikiwa ataonekana kwa mfano ana mimba. Pia mwanaume anaweza kuruhusiwa na mahakama kuoa akiwa na umri wa miaka chini ya 18 lakini lakini si chini ya 16 kama ataonyesha kuelewa jukumu lake kama mtu mzima. Lakini hii ni pale ambapo kuna tatizo kama la kumpa msichana mimba ndipo mahakama inaweza ikatoa idhini. Katika ombi la kuoa la SHABIRI A. M. VIRJI (1971) HCD NO. 407 la Mahakama Kuu ya Tanzania, mwombaji alikuwa na miaka 16 lakini alimpa mimba binti wa miaka 18. Mahakama katika kuchunguza ombi la mvulana la kuoa ilitoa kibali kwa sababu wote wawili walipendana sana na wazazi wao hawakuwa na kipingamizi cha wao kuoana.

MFUNGISHAJI NDOA KUTOKUWA NA MAMLAKA:
Kama wanaofunga ndoa wanajua wazi kuwa anayewafungisha ndoa hana mamlaka hayo na kwa makusudu wakakubali awafungishe ndoa basi ndoa hiyo itakuwa ni batili. Mfungishaji ndoa ili kuwa na mamlaka anapaswa kusajiliwa na Msajili Mkuu wa Ndoa na kupewa leseni ya kufungisha ndoa.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment