FEBRUARI
14 ipo njiani, kwa hiyo ile Siku ya Wapendao imesogea. Kwangu, naamini
kuwa ili sherehe hiyo iwe na maana ni lazima watu wakaelimika kuhusu
wivu, kwani migogoro mingi katika uhusiano wa kimapenzi husababishwa na
wivu.
Valentine’s Day siyo siku ya migogoro. Inapendeza kila mtu atibu
majeraha ya uhusiano wake mapema ili ikiwadia amani iwe inatawala. Ni
siku ya kufurahia maelewano na upendo wenu, muitumie kupeana zawadi na
kukumbusha matukio mazuri ambayo mmewahi kuyapitia.Haitavutia siku hiyo mkigombana, mtashangaza kwa maana asilimia kubwa ya wapendanao watakuwa kwenye furaha isiyo na kifani. Sasa basi, kuhakikisha amani inatawala, tafuta suluhu na mpenzi wako mapema (kama kuna mgogoro), halafu elimika kuhusu wivu, maana wenyewe ndiyo chokochoko.
0 comments:
Post a Comment