OMOTOLA AVUNJA REKODI NIGERIA YA KUWA NA MASHABIKI WENGI

Mwigizaji mahiri wa filamu nchini Naijeria amevunja rekodi kubwa ambayo inathibitisha kuwa ana mashabiki wengi mitandaoni na hii ni baada ya kuwa mtu maarufu wa kwanza wa nchi hiyo kuwa na mashabiki zaidi ya milioni moja katika ukurasa wake wa facebook pekee.

Kwa sasa idadi kamili ya watu ambao wamependa ukurasa wa mwanadada huyu ni 1,001,822  na bado mashabiki wake wanaendelea kuongezeka kwa kasi kutokana na mwanadada huyu kufanikiwa kuongeza wigo wa fani zake ndani ya muziki, filamu na vipindi vya televisheni.

Hii ni kama zawadi kubwa kwa Omotola ama Omosexy kama anavyopenda kufahamika hasa katika kusherekea kutimiza miaka 34 tangu kuzaliwa kwake Februari mwaka huu.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment