MSANII
wa filamu Tanzania Jacklin Wolpa anaamini mafanikio hutokana na
juhudi, kujituma pamoja na kutimiza malengo yako uliyojiwekea kwa
kipindi ulichokusudia
Msanii huyo wa filamu alielezea maisha yake yako nje ya Tasnia ya filamu alipokutana na mwandishi wa safu hii
Wolpa mbali na kuigiza pia yeye ni mcheza netiboli katika timu ya bongo
movi akiwa anachukua nafasi ya mfungaji 'GS' huku akiwa tishio kwa timu
pinzania kwa uwezo alionao na jinsi anavyoweza kutumia urefu aliokuwa
nao kwa kufunga magoli mengi
Alianza kucheza netiboli akiwa shuleni na huko ndipo alipopata ujuzi wa
mchezo huo ambapo mpaka sasa ameweza kuwa tishio kwa kuumudu mchezo huo
na kuweza kuisababishia ushindi kwa timu anayoichezea
Alisema kuwa anapata muda wa kutosha kufanya mazoezi kila siku jioni na
asubuhi hivyo mazoezi yanamsaidia kujenga mwili wake pia na kumpa pumzi
zinazomsaidia kucheza kipindi chote bila ya kupumzika mpaka mwisho wa
mchezo
Aliendelea kusema kuwa kwa upande wake anathamini sana mazoezi kwani
yanamfanya kuzidi kuwa imara na pia hutumia mazoezi kwake ni kama dawa
ya kuondoa uchovu katika mwili wake
Wolpa aliweka wazi kuwa kama ingekuwa si muigizaji basi angekuwa
mchezaji mzuri wa netiboli na angeongeza nguvu katika hilo na kuweza
kuchezea timu kubwa na anaamini kuwa angefanya vizuri kwenye upande huo
Anaeleza kuwa hatoweza kusahau siku alipoumia vidole vya mikono kwenye
mechi iliyokuwa inachezwa katika viwanja vya Leaders Club na aliweza
kuendelea kucheza mchezo huo na hatimaye waliibuka washindi katika mechi
ya kujipima
Mbali na kucheza netiboli pia msanii huyo ni bingwa wa kuogelea, huku
akidai kuwa muda wake mwingi wa mapumziko anautumia kuogelea ili kuweka
mwili wake imara
Aliongezea kuwa mara nyingi huwa anaratiba ya nini afanye muda gani na
kipi kifanyike wakati gani hiyo ndiyo moja ya kitu anachoamini kuwa
kinampa mafanikio makubwa katika maisha yake
Wolpa alisema huwa hapendi kuwa na makundi ya watu hivyo hawezi kuamua
kwenda kukaa bar kama hana kazi ya kufanya kwa sababu ratiba yake
inakuwa imejaa muda wote ule
Wolpa ambaye pia alikuwa anafanya biashara ingawa sasa anajipanga
kuianzisha tena biashara yake ili maisha yake yaendelee kuwa yenye
mafanikio kwa juhudu anazozifanya
Aliongezea kuwa anapenda kusoma vitabu muda wa mapumziko zaidi kuliko
kwenda kukaa bar na marafiki ambao kwake anahisi laba hawana mafanikio
ingawa si kila rafiki ni mwema au ni mbaya hivyo kwa upeo wa kiubinadamu
huwezi kutambua hilo kwa haraka
Anasema kuwa kusoma vitabu kunamsaidia kumjenga kiuwezo na fikira pia
inamuongezea kuwa mbunifu hususani katika kazi zake za sanaa
Wolpa ni msanii wa filamu ambapo alianza kuigiza mwaka 2009 na filamu
iliyomtambulisha ni Amazangu amazao kwa sasa anatamba na filamu nyingi
ikiwemo ya Ndoa yangu aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba
0 comments:
Post a Comment