
.
Ukijaribu kupata picha ya jinsi tukio lilivyotokea na hasa kwa umri wao mdogo yani ndio inakua tabu na chanzo bado hakijajulikana.
Yani ni kwamba katika shule moja huko Bronx New York Marekani kuna mwanafunzi mmoja wa darasa la tatu kampa kichapo mwanafunzi mwenzake wa darasani kisha akamfunga na pingu kwenye chuma ukutani shuleni alafu akamalizia kwa kumuibia dola 5.
Polisi wametangaza kumsaka huyo mtoto ambae inaashiria hata akija kuwa na umri mkubwa atakua mwepesi wa kufanya uhalifu au kudhuru wengine, ndio ujiulize akija kupata bastola siku moja katika nchi hiyo ambayo upatikanaji wa bastola ni mrahisi itakuaje?
0 comments:
Post a Comment