
"Yaa! ni kweli kuwa nimeamua kuondoka Mtanashati kuepuka ubabaishaji mkubwa uliopo ndani ya kundi hilo ambalo mkurugenzi wake amekuwa akiwanyima nafasi wasanii wengine na kuwapendelea baadhi akilenga zaidi kujinufaisha kupitia majina ya wasanii hao" alisema Amazon
Akiendelea zaidi nyota huyo wa singo ya checherumba alisema kuwa amechoshwa na 'uditeta' wa mkurugenzi unaofanywa na mkurugenzi wa kundi hilo ikiwemo hatua ya kuwataka wasanii walio ndani ya kundi hilo kutia saini mkataba wa Milele utakaowafanya kuwajibika ndani ya kampuni hiyo maisha yao yote.
"Awali nilitakiwa kusaini mkataba wa 'milele' ambao unakutaka kufanya kazi maisha yako yote ndani ya kundi kitu ambacho binafsi nilikitaa kwa kuwa sijawahi kuona mkataba wa aina hiyo sehemu yoyote ile ingawa ajabu ni kuwa kuna baadhi ya wasanii wenzangu wameukubari" alisema Amazon.
0 comments:
Post a Comment