jack p
STAA
wa Bongo anayetesa kwenye mitindo, Jacqueline Patrick anakabiliwa na
msala wa kumtwanga na chupa nusu kumuua mrembo anayejulikana kwa jina la
Hafsa Sasya, Risasi Mchanganyiko linanashuka nayo.
Habari
zilizopenyezwa na chanzo chetu kutoka eneo la tukio zinasema kwamba,
ishu ilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Januari 26, mwaka huu ndani
ya Ukumbi wa Elements Lounge uliopo Masaki, Dar.
CHANZO KINATIRIRIKA
Huku
sharti la kutotajwa jina lake gazetini likisisitizwa na chanzo hicho,
kilisema: “Unajua yule dada (Hafsa) anasoma Kurasini na anaishi
Kijitonyama, namfahamu vizuri sana. Walipokutana na Jack pale ukumbini
palitokea kutokuelewana kidogo.
“Baada
ya muda hali ikawa sawa, watu wakajua yamekwisa. Jack akaenda zake
chooni, aliporudi alikuwa na chupa na kwenda kumpiga nayo Hafsa.
Mabaunsa wakamwondoa Jack ukumbini na kumwingiza Hafsa kwenye gari lake
kwa lengo la kumpeleka hospitalini. Kilichoendelea hapo sijui.”
PEKUPEKU ZA RISASI
Mwandishi
wetu aliingia mzigoni rasmi na kuanza kuichimba kwa kina habari hiyo
ambapo alipata uhakika wa kutokea kwa tukio hilo na Jack kufikishwa
katika Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo alifunguliwa kesi yenye jalada
namba OB/RB/1678/13 KUJERUHI.
Baada
ya kujiridhisha kwa hilo, zoezi lililofuata lilikuwa ni kuwatafuta
wawili hao ili waeleze wanachokijua kuhusu tukio hilo. Wa kwanza
kupatikana alikuwa ni Jack.
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA JACK
“Ni
kweli kulitokea ugomvi siku ile...na ni kweli nilihojiwa na Polisi wa
Kituo cha Oysterbay, lakini nimetoka kwa dhamana na kesi imekwenda
mahakamani.”
HUYU HAPA HAFSA
“Mimi
na Jack tulikuwa marafiki lakini nashangaa amenipiga na chupa bila
sababu. Nimeshonwa nyuzi tatu. Siku ile alinikuta nimesimama na rafiki
yangu mara akanipiga kikumbo kisha akaenda chooni, aliporudi akanikumba
tena, nilipomuuliza ikawa kosa; akanipiga na chupa.
“Imeniuma
sana maana amenipa jeraha usoni mwangu bila sababu ya msingi, maana
sina ugomvi naye. Kwa sababu hili suala lipo mikononi mwa sheria,
naamini itachukua mkondo wake.”
0 comments:
Post a Comment