MAMBO MANNE KUHUSU 'DIAMOND PLATINUMZ' AMBAYO HUYAJUI... MWENYEWE AFUNGUKA...

Mkali wa Bongofleva kwa sasa, Diamond Platnumz a.k.a 'Sukari ya Warembo' jana kwenye The Mboni Show inayorushwa kwenye kituo cha Television cha EATV alifunguka mambo manne ambayo nina uhakika wengi wetu hatukuyajua:

1. Diamond alihangaika sana mpaka kufikia hapa alipo sasa, alipitia magumu mengi sana katika maisha, yakiwemo kuuza m
itumba, kuuza mafuta ya taa na kufunga kufuli za mabegi lakini tuzungumzie inshu ya mitumba. Kumbe wakati anauza mitumba pale magomeni, Diamond alishawahi kuwauzia wakina Ally Kiba, TID na Bob Junior mitumba hiyo kwenye Goli lake. Lakini anaamini wasanii hao hawakumbuki kama yeye ndio aliwauzia, ila Bob Junior pekee ndio anajua.

2. Kutokana na maisha magumu aliyopitia, Diamond anaamini kwamba mademu wengi walimuacha na kumtenda kwa sababu hakuwa na kitu. Sasa kumbe nyimbo ya 'Kamwambie' alimwimbia demu ambaye ndiye demu aliyemtenda na hatomsahau maishani kwake, demu mwenyewe anaitwa Sarah. Mpaka sasa hajui tena alipo wala anafanya inshu gani.

3. Wote tunajua kwamba Wema Sepetu alikua mpenzi wa Diamond Platnumz, na tunajua kwamba mwanadada huyo kinamna flani kamsaidia sana Diamond hata hivyo Diamond mwenyewe katika watu (wanawake) anaowashukuru basi hakusita kumtaja Wema na Jokate. Sasa kumbe Wema amemtungia Diamond mistari kwenye huu wimbo wake mpya wa 'Nataka Kulewa'... 

4. Diamond mpaka sasa amefanya Shows nyingi sana, na mpaka sasa mwenyewe anadai analipwa 10 Million shilingi za kitanzania kwa show moja. Sasa jamaa kafunguka kwamba Show ya kwanza kabisa kufanya ilikua Fiesta na alilipwa Tsh. Elfu hamsini (50,000/=) tuu...

Did you know all these?
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment