AMINI KUMTAMBULISHA MPENZI WAKE MPYA SIKU YA FIESTA YA DAR TAREHE 6 OCT

BAADA ya kusumbuka sana na mapenzi yakiwemo ya kumpenda staa, msanii Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, ametangaza kuwa Octoba 6 mwaka huu siku ya tamasha la Fiesta, atamtambulisha mpenzi wake ambaye, anayechukua nafasi iliyoachwa wazi na Linah.

Kwa hakika utambulisuho huo utakuwa wa aina yake kwani mashabiki wake wengi wanajua jamaa bado anamzimia Ndege Mnana huku wakiwa hawaelewi kitu kilichowafanya hadi wakaachana ingawa bado wana mahusiano mazuri kwenye kazi.

Amini aliumpa mtandao huu mchongo huo ili kuwataliafu mashabiki wake kuwa alikuwa kimya kwenye suala zima la mapenzi baada ya kuumizwa sana, lakini sasa anaamini ni wakati muafaka wa kumtambulisha kimwana wake.

Alisema kuwa mpenzi atakayemtambulisha siku hiyo ndiye mke mtarajiwa kwani haoni sababu ya kuendelea kuumizwa na mapenzi wakati muda wa kuvuta jiko umekaribia.

“Sihitaji kumtambilisha kama mpenzi bali ni kama mke kwa sababu naamini anavyonipenda ni kiasi cha kujivunia kwa sababu mara zote huwa nazungumza naye mambo ya ndoa na yupo radhi kuishi na mimi kwa shida na raha,” alisema Amini.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment