MAY D ATIMULIWA NA P Square



P Suare na Akon.
Unakumbuka ile kolabo ya P Square na Akon inaitwa Chop my money ambayo ilimfanya May D kuwa staa zaidi baada ya kuongezwa kuwa mtu wa nne kusikika kwenye hiyo single?
kama hufahamu May D ni msanii wa Nigeria ambae alisainiwa kuwa chini ya lebo inayomilikiwa na P Square (Square Records) ambapo ni siku kadhaa zimepita toka lebo hiyo itangaze kwamba haimuhitaji tena na wala hayuko tena chini yao.
Leo mtandao wa Naijag umeripoti kwamba May D ambae alitimuliwa na lebo hiyo wiki kadhaa zilizopita yuko kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na wanasheria wake ili awashitaki P Square kwa kuvunja mkataba kiholela.
May D anasema taarifa za kutimuliwa kwake alizipata kwenye blogs na magazeti kama walivyopata watu wengine na kwamba hakupewa taarifa zozote za kiofisi kama inavyopaswa, hiyo ndio sababu inayomfanya awashitaki P Square akiwemo kaka yao mkubwa Jude Okoye ambae ndio alitangaza kuuvunja mkataba wa May D.

.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment