
Staa wa Bongo movies na Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ Zuwena Mohammed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuh Mziwanda.
Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limemfungia Shilole kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.
“Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza
uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha
utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili‘
‘BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya
na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia
maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini
usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa
maelezo yako‘
‘Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye
onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya
30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa
kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha
kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja,
kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote
utakayeshirikiana naye ‘
Aidha kibali chako cha kuendesha shughuli za sanaa kimesitishwa tokea tarehe ya barua hii hadi pale itakavyoamuliwa vinginevyo.


0 comments:
Post a Comment