NAHODHA wa Ghana, Asamoah Gyan amesema hatopiga
penalti katika muda wa kawaida wa mchezo wakati wa fainali za Mataifa ya
Afrika zitakazoanza kutimua vumbi nchini Afrika Kusini wiki ijayo.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27, alikosa penalti
iliyowanyima Ghana nafasi ya kufuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Dunia
2010 na akakosa tena kwenye nusu fainali ya Kombe la Afrika mwaka jana.
Baada ya kitendo hicho mshambuliaji huyo alijikuta
kwenye wakati mgumu kutoka kwa mashabiki na kusababisha ajiuzulu
kuichezea timu ya taifa kwa muda, lakini sasa Gyan ameamua kutopiga
kabisa penalti.
“Nimeamua kutokuwa mpigaji wa penalti wa timu ya taifa,” alisema.
“Wachezaji wengi mashuhuri wanakosa penalti kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Diego Maradona. Ikiwa siku yako mbaya utakosa.
“Lakini nilishasema mwezi moja uliopita kuwa sitopiga tena penalti. Kabla ya mama yangu hajafariki mwezi Novemba aliniambia nisipige tena penalti.”

Miaka miwili iliyopita Gyan alishindwa kufunga
penalti dhidi ya Uruguay kwenye dakika za mwisho za mchezo wa robo
fainali ya Kombe la Dunia, na kama wangeshinda mchezo huo basi Ghana
ingekuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufuzu kwa nusu fainali kwenye
historia ya mashindano hayo.
Pia, Februari 2012, Gyan alikosa penalti iliyoinyima nchi yake kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Zambia.
Pia, Februari 2012, Gyan alikosa penalti iliyoinyima nchi yake kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Zambia.
Ghana itaanza kampeni zake kwa kucheza na DR Congo kabla ya kuivaa Mali na Niger zote zikiwa Kundi B.
0 comments:
Post a Comment