Baada ya kukumbwa na kashfa ya ubaguzi, Justin Bieber amrudia Mungu na kubatizwa.
Katika harakati za kujirudisha kwa jamii yake na kuomba msaada wa Mungu tangu akumbwe na kashfa ya kutoa maneno ya kibaguzi, Nyota wa muziki mwenye makazi yake nchini Marekani Justin Bieber amechukua uamuzi wa kubatizwa kya kwa madai ya kutaka kusafisha dhambi zake.
Nyota huyo alilazimika kuomba msamaha baada ya video inayomuonyesha akitania kwa maneno ya kibaguzi kuvuja mtandaoni.
Hivi sasa Bieber amekuwa akitumia muda mwingi jijini New York na mchungaji ambaye amekiri kuwa wamekuwa wakitumia muda mrefu na mwanamuziki huyo kujifunza masomo ya biblia.
Justin alitaka kubatizwa kama sehemu ya kujiunga na ukristo lakini alikuwa akihangaika kutafuta kanisa litakalomtunzia siri yake hiyo kwasababu amekuwa akifuatiliwa sana kwa karibu na vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment