VIDEO YA NISHIKE KUTOKA KWA SAUTI SOL YA FUNGIWA

Screen Shot 2014-04-30 at 2.08.18 AMMpaka sasa video hii imetazamwa zaidi ya mara laki moja na elfu 30 kwenye mtandao wa Youtube toka ianze kuonyeshwa April 29 2014 ikiwa ni video ya kipekee na ya kiwango kingine cha juu tofauti na ilivyozoeleka kwa Sauti Sol.
Mtandao wa Kenya ghafla.co.ke umeripoti kwamba imefahamika video hii imezuiwa kuchezwa kwenye TV stations mbalimbali za Kenya kwa sababu imevunja maadili.
Kwenye Mdundo Awards jana usiku Bien Aime wa Sauti Sol alisema mwanasheria wao anashughulikia ishu ya kufungiwa kwa video yao ambayo imeambiwa inachochea ngono kutokana na uwazi wa wanaookenana ndani yake.
Hii itakua video nyingine iliyochukua headlines zinazofanana na ile ya P Unit ‘you guy’ ambayo ilifungiwa na CITIZEN TV kwa sababu ya mrembo alieliachia umbo lake kwa sana.
Hata hivyo kwenye tuzo za Channel O 2013 P Unit waliiambia succi na succi tv‘video yetu inaonyeshwa sana bado na hata waliosema wameifungia ndio wanatuita hapo kwa interview…, hii ni ile video mzazi wako anakwambia usione alafu yeye usiku anaitazama’

SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment