Asema umehodhiwa na wanasiasa na kutahadharisha usipoangaliwa unaweza kuzaa machafuko.
Dodoma. Mwanazuoni na
Mwanasheria nguli, Profesa Issa Shivji ameuponda mchakato wa Katiba
Mpya kuwa umehodhiwa na wanasiasa na kutahadharisha kuwa usipoangaliwa
vizuri unaweza kusababisha machafuko.
Aliyasema hayo jana mjini hapa alipokuwa akitoa
mhadhara kwa Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dodoma, (Udom). Mhadhara huo
uliandaliwa kama sehemu ya mafunzo kwa ajili ya wanafunzi wanaojiandaa
kuhitimu masomo yao (Convocation ).
Profesa Shiviji ambaye alitumia saa 1.15 kutoa
mhadhara wake juu ya mchakato wa Katiba, alisema Bunge la Katiba lipo
juu ya Bunge la Kawaida.
Alisema katika historia ya Tanzania imewahi kuwa
na mabunge mawili yaliyoandaliwa kupata Katiba, lakini yote hayakuwa na
wabunge waliochaguliwa.
“Tukiangalia katika historia hatukuwahi kuwa na
Bunge la Katiba ambalo lilichaguliwa na wananchi. Safari hii tulikuwa na
nafasi ya kuwa na Bunge ambalo lilichaguliwa na wananchi lakini kwa
bahati mbaya hakuna nafasi ya kufanya hivyo ,”alisema.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
wabunge wote 357 na Wawakilishi 81 watakuwa ni wabunge wa Bunge Maalumu
la Katiba huku mashirika yasiyo ya kiserikali yakipewa wawakilishi 20.
Wajumbe wengine ni vyama vya siasa vyenye usajili
wa kudumu 42, wawakilishi wa taasisi za elimu ya Juu 20, watu wenye
mahitaji maalumu (20), vyama vya wafanyakazi (20), wafugaji (10), wavuvi
(10), wakulima (20) na makundi mengine yenye mahitaji muhimu ni
wawakilishi (20).
Profesa Shivji alisema Bunge la Katiba litakuwa
na jumla ya wabunge 639, ambapo 438 asilimia 69 ya wabunge wa Bunge
hilo wanatokana na vyama vya siasa.
Alisema kati ya wabunge hao kutoka vyama vya siasa asilimia 52 ni Wana-CCM na asilimia 16 ni kutoka vyama vya upinzani.
“Katika wajumbe 42 watatokana na vyama vya
kisiasa, kwa hivi itafanya jumla ya wabunge la Katiba ambao watatokana
na vyama vya siasa kuwa ni asilimia 75;
“Kama hesabu zangu ni sahihi ama zinakaribia
wabunge wanaotokana na CCM watakuwa ni asilimia 63, wapinzani asilimia
27 na wasiokuwa na chama ni asilimia 10,”alisema.
0 comments:
Post a Comment