Na Mwandishi Wetu
SAKATA
la wasichana wawili, Kate Gee (18) na Kristie Trup (18), raia wa
Uingereza ambao walimwagiwa tindikali wakiwa katika matembezi Mtaa wa
Shangani, visiwani Zanzibar Agosti 8, mwaka huu, limeingia sura nyingine
baada ya sababu ya tukio hilo kuanikwa.Habari za chini kwa chini zinadai kuwa namna ya uvaaji ilichangia wasichana hao kutendewa ukatili huo wa kutisha ambapo ilisemekana waliofanya hivyo walikuwa wanatoa onyo kwa wengine.
MWEZI MTUKUFU WATAJWA
“Wale jamaa (waliowamwagia tindikali Wazungu) lengo lao ni kuwapa fundisho na wengine pia ili suala la kukiuka mavazi mwezi mtukufu lisijirudie,” alisema mtoa habari wetu.
Habari zaidi zilidai kuwa kundi la watu wachache wenye imani kali ya Kiislamu (si Waislamu wote) ndiyo walitekeleza ukatili huo kwa sababu wasichana hao siku ya tukio walivaa mavazi yasiyoendana na kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
“Hakuna lingine, wale waliponzwa na mavazi, unajua hapa Zanzibar tunaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, akitokea mtu anakwenda kinyume lazima aadhibiwe,” alisema mkazi mmoja wa kisiwani humo huku akikataa kutaja jina lake.
DALILI ZILIANZA MAPEMA
Ilizidi kudaiwa kwamba, siku chache kabla ya tukio, mmoja wa wasichana hao aliwahi kupigwa makofi kisa kikidaiwa alikuwa akitembea mtaani huku akiimba katika kipindi cha mfungo wakati watu wapo kwenye swaumu.
ZANZIBAR BADO NI SALAMA KWA WAGENI?
Kufuatia tukio hilo, mhariri wa masuala ya utalii wa Gazeti la Mirror la Uingereza, Nigel Thomson aliwaambia watalii kutoka Uingereza kwamba Zanzibar bado ni sehemu salama kwa kwenda kutalii ilimradi kuheshimu namna ya kuvaa katika nchi yenye umakini wa mavazi.
Naye Marc Trup, baba wa Kristie alisema watoto hao walishaonywa juu ya mavazi.
MASTAA WA BONGO WALIWAHI KUONJA JOTO LA JIWE KWA MAVAZI
Julai mwaka jana, staa wa filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ alinusurika kuvuliwa nguo kufuatia kuvaa kimini. Ilikuwa ndani ya mfungo.
Tukio hilo lilimkuta msanii huyo maeneo ya Darajani, kisiwani humo. Ilimlazimu kukimbilia dukani na kununua gauni maarufu kwa jina la ‘dela’.
Kama vile haitoshi, mastaa wengine wa Bongo, Wema Sepetu, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Halima Yahya ‘Davina’, Snura Mushi na Sabrina Rupia ‘Catty’ waliwahi kukumbwa na dhahama kubwa kuhusu mavazi.
Ilikuwa Mei, mwaka jana walipokwenda kisiwani humo kumpa kampani msanii akwenye uzinduzi wa filamu yake iitwayo Toba, walipigwa ‘stop’ kuingia Hoteli ya Bwawani kwa sababu ya kuvaa nusu utupu, ikabidi wakanunue madela ndipo waliporuhusiwa kupita getini.
KUMBE SI MAVAZI TU
Akizungumza juzi kwa sharti la kutotajwa jina gazetini, sheha mmoja (kiongozi wa serikali ya mtaa) kisiwani humo alisema kwa kawaida, mwezi mtukufu kuna mambo huwa yanatakiwa kusitiriwa.
“Hapa kwetu (Zanzibar), mwezi wa kufunga swaumu mtu hatakiwi kula hadharani wala kulewa. Lakini walichotendwa wale mabinti ni kibaya sana, mimi nakilaani, Uislamu wetu hausemi vile, walitakiwa kuelimishwa kwa sababu inajulikana wao ni wageni wa desturi ya hapa,” alisema.
KATE, KRISTIE WALIKUWA AKINA NANI?
Kate na Kristie walikuwa walimu wa kujitolea katika Shule ya Mtakatifu Monica inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana Jimbo la Zanzibar.
Walisafirishwa kwenda Uingereza Ijumaa iliyopita baada ya kupewa matibabu ya awali katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar.
Juhudi za kumtafuta Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Said Ali Mbarouk kuzungumzia sakata hilo ziligonga mwamba baada ya simu yake kutopatikana hewani kila alipopigiwa.
KUTOKA DAWATI LA WIKIENDA
Ni tukio baya sana, Kate na Kristie huenda wakawa wameondoa mapenzi yao kwa nchi ya Tanzania hata kama waliipenda kupita kiasi mpaka wakajitolea kuja kufundisha.
Ni vyema jeshi la polisi likafanya juu chini kuwakamata wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa kosa la kujaribu kuua ili kujiwekea mazingira safi kwa jamii za kimataifa.
Kufuatia tukio hilo tayari Rais Jakaya Kikwete ameshatoa tamko la kulaani
0 comments:
Post a Comment