SHARE THIS STORY
Suarez alitarajiwa kufanyiwa vipimo baada ya
kugundulika kuwa na tatizo la mguu, jambo lililomfanya kukosa mchezo wa
kirafiki wa kimataifa dhidi ya Valerenga mjini Oslo jana usiku.
Arsenal bado imesimama imara kutaka kumsajili
nyota huyo ingawa dau lao pa Pauni 41 milioni limekataliwa. Tajiri Henry
amesisitiza kwa kusema klabu yake ya Liverpool haiuzi ila inanunua.
“Luis Suarez ni mchezaji nafasi ya kwanza
Liverpool, kinachozungumzwa kwa sasa hakilingani na thamani yake, labda
mtu aje na ofa inayoeleweka yenye kumpa thamani,” alisema Henry. “Hatuna
dhamira ya kumuuza mmoja kati ya wachezaji bora duniani kwenda kwa
wapinzani wetu. Sera yetu ni kununua siyo kuuza.”
Lakini mwenyewe Suarez, kwa mara nyingine tena
ameifungua nia yake ya kutaka kuondoka Kops. Suarez alisema: “Nina miaka
26, nahitaji kucheza Ligi ya Mabingwa.
“Tulikubaliana kwamba nitaondoka kipindi hiki kama Kops hawatapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
“Nilijitolea na kufanya niliyoweza msimu uliopita, nachokihitaji kwa sasa ni Liverpool kuheshimu makubaliano yetu ya awali.”
Aliongeza: “Mwaka jana nilipata nafasi ya kujiunga
na moja kati ya klabu kubwa Ulaya, lakini nilibaki kwa makubaliano
kuwa, kama hatuapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa, nitaondoka.”
Arsenal wamefanya majaribio mawili ya kutaka kumsajili Suarez, lakini yote yamepigwa chini.
“Sidhani uamuzi wangu wa kuondoka ni kama
nimeisaliti klabu yangu, muhimu ni kuheshimu makubaliano ya mwaka mmoja
uliopita,” alisema zaidi.
0 comments:
Post a Comment