Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wibrod Slaa akiwasili katika viwanja vya Kilombero Jijini Arusha
Wananchi wakifuatilia kwa makini maoni mbalimbali
Baadhi
ya wananchi wakinyoosha mikono kuashiria kukubaliana na maoni ya
mwenzao aliyependekeza vyeo vya ukuu wa wilaya na mkoa kuondolewa kabisa
kwenye katiba mpya na badala yake viongozi wa ngazi hizo wachaguliwe na
wananchi wa maeneo husika. Zoezi hilo la kutoa maoni lilikuwa
linasimamiwa na Dk Slaa
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr Wilbroad Slaa
akizungumza na wananchi wa Jijini Arusha jioni ya leo katika muendelezo
wa Mikutano ya wazi ya Mabaraza ya Kitaasisi ya Chadema kukusanya maoni
ya Katiba Mpya kwa upande wa Chadema kama taasisi kamili.
Dr Slaa
kwa siku ya leo amefanikiwa kufanya mikutano miine ya wazi Mkoani
Arusha na baadae kushiriki katika kikao kingine cha mabaraza hayo cha
ndani kilinachoendelea katika hoteli ya New Arusha.
Katika
mikutano hiyo Dr Slaa ameambatana na wanasheria wa chama akiwemo Mabere
Marando pamoja na viongozi wengine kutoka makao makuu akiwemo mjumbe wa
Kamati Kuu Dr Kitila Mkumbo.
Wananchi mbali mbali walipata fursa
ya kutoa maoni yao hadharani katika mjumuiko huo uliohudhuriwa na maelfu
ya wananchi, na kujaza eneo la wazi katika viwanja vya Kilombero Jijini
hapa.
Mzee Ole Kisambo, ambaye aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mgaharibi akitoa maoni yake kwa Dk Slaa.
Mzee OleKisambo, ambaye aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mgaharibi akitoa maoni yake kwa Dk Slaa.
Mwanasheria
wa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama, Wakili Mabere Marando
akichambua baadhi ya vifungu vya rasimu ya Katiba inayokusudiwa kutolewa
maoni na wananchi. Marando amesema kwa upande wa Chadema wanaunga mkono
zaidi ya asilimia 80 ya mambo yaliyomo katika rasimu hiyo iliyoandaliwa
na Tume inayoongozwa na jaji Warioba.
Mratibu
wa vikao vya mabaraza ya Chadema, mh Mwita Waitara akisalimia wananchi
kabla ya kumkaribisha Wakili Mabere Marando ambye pia alimkaribisha Dk
Slaa
Wanasheria
vijana wakiwafafanulia wananchi vipengele mbalimbali vya rasimu ya
Katiba. Mwenye suti ni James Lyatuu na mwenye tisheti ya mistari ni
Mathias Lyamunda
Walemavu pia walipata nafasi kuwasilisha maoni yao…
Mmoja wa kina dada waliojitokeza kutoa maoni yao pia
Kulikuwa na fomu nyingi zilizogawiwa kwa wananchi wengine kutoa maoni yao kwa kuandika kama huyu
Jukwaa kuu nao walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa kujaza fomu maalum
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kutoa maoni yao kuhusiana na rasimu ya Katiba Mpya
Viongozi
wote na wananchi walikaa kimya kwa muda wa dakika moja kama ishara ya
kumbukumbu za wananchi waliouwawa kwa kulipukiwa na mabomu katika
mkutano wa chadema jijini Arusha kwenye uwanja wa Soweto Juni 15, 2013.
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akibadilishana
taarifa na viongozi wa Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini, wakati huo
huo Marando akizungumza na Ally Bananga.Chanzo:Hakingowiblog
0 comments:
Post a Comment