Akizungumza Daktari Mohammed Jawad, ambaye
anawaangalia kwa ukaribu zaidi wagonjwa hao, alisema kwamba Katie ambaye
aliathirika zaidi anahitaji kupandikizwa ngozi nyingine.
Alisema kutokana na majeraha ambayo aliyapata
mwalimu huyo aliharibika ngozi yake hivyo anahitajika kupandikizwa ngozi
nyingine ili arudi katika hali yake ya kawaida.
“Vipimo vilionyesha kwamba mgonjwa huyo alipata majeraha makubwa hivyo anahitajika kupandikizwa ngozi nyingine,” alisema.
Kwa sasa walimu hao wanapata huduma ya matibabu
katika Hospitali ya Chelsea and Westminster iliyopo London walikopelekwa
wakitokea Tanzania wiki iliyopita.
Familia ya wagonjwa hao imeonekana kuwa karibu
zaidi na mabinti hao baada ya kuwapeleka moja kwa moja hospitalini hapo
kwa matibabu zaidi.
Msemaji wa hospitali hiyo alisema kwamba wagonjwa
hao wanaendelea na matibabu vizuri na hali zao siyo mbaya sana kama
ilivyokuwa awali.
“Wagonjwa wanaendelea vizuri na matibabu na kila
siku familia zao zinakuja hapa kuwaona na kuwafariji, kwa kweli hali zao
ni nzuri,” alisema msemaji huyo wa hospitali hiyo.
Siyo mara ya kwanza
Mtandao mmoja wa kijamii unaofahamika kwa jina la
www.ziro99.blogspot.com umeandika taarifa kwamba walimu waliomwagiwa
tindikali mjini Zanzibar walishawahi kumwagiwa tena.
Habari za kuaminika zilizopatikana kupitia mtandao
huu zilifichua kwamba mmoja wa walimu hao alishawahi kushambuliwa
wakati akiwa kisiwani humo wiki mbili zilizopita.
Kwa mujibu wa mmoja wa marafiki zao, akizungumza
kupitia katika mtandao huu Oli Cohen, mwenye miaka 21, alisema: “Katie
alishambuliwa wiki mbili zilizopita na mwanamke mmoja wa Kiislamu baada
ya kuimba wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.”
0 comments:
Post a Comment