WAZIRI MKUU PINDA AKIWA HOSPITALI AKIMJULIA HALI MBUNGE WA CHADEMA ALIE PATA MAJERAHA BAADA YA BOMU KULIBUKA


Arusha. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema bomu lililolipuliwa katika mkutano wa Chadema ni la kijeshi na limetengenezwa China.
Akizungumza mjini hapa jana, Pinda alisema uchunguzi unaendelea kujua bomu hilo limefikaje kwenye mikono ya waliohusika kwani uzoefu unaonyesha kuwa hutumiwa na wanajeshi kujihami wakiwa katika makabiliano na maadui vitani.
“Ingawa uchunguzi unaendelea, lakini inawezekana bomu hilo limeingizwa nchini na wahalifu wasiojulikana kupitia njia za panya za mipakani,” alisema Pinda.
Serikali kusimamia mazishi
Katika hatua nyingine, Serikali imetangaza kwamba itasimamia mazishi ya watu waliopoteza maisha kutokana na shambulio hilo.
Hatua hiyo imekuja huku Chadema nacho kikiwa kimetangaza kushughulikia mazishi ya wananchi hao kwa kuwa walifariki katika shambulio lililotokea kwenye mkutano wao.
Waziri Mkuu, jana alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo kusimamia shughuli zote za misiba hiyo, agizo ambalo wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema ni kama kuipokonya Chadema dhamana ya kusimamia shughuli za mazishi hayo.
Juzi jioni, Mbowe aliwaambia wananchi na wafuasi wa Chadema katika Viwanja vya Soweto kuwa chama chake kitagharimia na kusimamia shughuli zote za kuaga, kusafirisha pamoja na 
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment