KIPAJI KIPYA CHA SWIZZ BEATS



Huu ni ubunifu wa aina yake ambao Swizz Beats ameamua kuutumia kwaajili ya kusapoti ama kupata fedha za kuendesha shughuli zake za kusaidia wenye uhitaji ndani ya Jamii.

Kwa kutumia 'bonet' za magari, Mwanamuziki/Producer huyu mkali ameamua kutumia kipaji chake kingine cha kutengeneza paintings 50 ambazo huziambatanisha na picha za watu maarufu - na kutoa collection ya kazi safi kabisa ya sanaa kama inavyoonekana katika picha hapa.

Kazi hizi za sanaa ambazo Swizz ametengeneza, ni kwaajili ya kuuza na moja ya kazi hii ina thamani ya zaidi ya dola 20,000 za kimarekani, ama zaidi ya shilingi milioni 30 za kitanzania.


Katika kusapoti mpango huu, tayari Jay Z amekwishanunua moja ya kazi hii ambayo Swizz ametengeneza maalum kwaajili yake, na pesa za mauzo ni kwaajili ya kusaidia moja ya shule ya sanaa ambayo Swizz anaipiga sapoti.


SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment