UNAMUELEWA T.I.D KWA KWELI YEYE SI ALIJITOA KAMA UNAKUMBUKA SAS NIAJE


Hatimaye Mnyama TID ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia suala la kukosa kutajwa kuwania tuzo za Kili mwaka huu na kudai anahisi amehujumiwa. Akiongea exclusively na Bongo5, TID amesema ameshangaa wimbo wake Kiuno kutoingizwa kwenye tuzo hizo ilhali ulifanya vizuri kwenye redio na kwenye TV.

“Waliniita before hata hizo nominations na nini, mimi nilikuwa safarini nikashindwa kufika na tayari nilishaongea na Kavishe tulikuwa gym tukakubaliana kwamba hizi issue ziishe sasa nashangaa kwenye nominations sijawekwa na wimbo wangu sijui maana yake nini,” amesema TID.

Amesema hawezi kuilaumu academy inayochagua nominations hizo kwakuwa hupelekewa majina.“Hapo kuna kauli imetoka ya mtu mwingine ambaye amekataza nisiwekwe,” amesisitiza.Amesema tayari alishakubali kuziweka tofauti zake na waandaji wa tuzo hizo pembeni ili kuanza ukurasa mpya lakini haelewi ni kipi alichowakosea mara nyingine.

“Kwanini sasa wasiniweke, nini kitu kibaya nilichofanya mimi? Nahisi kuna mchezo kwasababu wimbo wangu ulitakuwa uingie kwenye categories kibao na ushinde sababu umehit sana mwaka jana.”
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment