SUMATRA WAAGIZWA KUANGALIA UWEZEKANO WA KUTOA LESENI KWA MAGARI AINA YA NOAH KUTOA HUDUMA YA USAFIRI



Waziri wa Uchukuzi Dk. HARRISON MWAKYEMBE ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kuangalia uwezekano wa kutoa leseni za Usafirishaji wa abiria kwa magari madogo aina ya NOAH.
Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Waziri MWAKYEMBE amesema kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu kuhusu kutoruhusiwa kwa magari hayo kutoa huduma katika maeneo yenye uhaba wa usafiri.Katika hatua nyingine Waziri MWAKYEMBE amesema huduma ya usafiri wa Treni kwa jiji la Dar es Salaam imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano na kuokoa muda kwa watumiaji wa usafiri huo ambapo amesema mpaka sasa jumla ya watu Elfu 15 wanatumia usafiri wa Tren kwa siku jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasilishwa kwa bajeti hiyo wabunge wamepata fulsa ya kuchangia ambapo mbunge wa Nkasi Kaskazini ALLY KESSY ameshauri hatua kali zichukuliwe kwa wote walioyafilisi mashirika ya Umma na kuweka pingu kwenye makaburi ya wale waliokufa.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment