Kamati ya mipango ya mazishi ya marehem Ngwea wametoa taarifa mpya kwamba mwili wa ndugu yetu Albert Mangwea utafika siku ya juma pili ya tarehe 2 / 6 saa nane mchana na sio siku ya jumamosi kama ilivyotaarifiwa hapo awali.
sababu za mwili wa Albert Mangwea kushindwa kufika jumamosi kama ilivyopangwa ni kutokana na watanzania waishio Africa Kusini, kuomba na wao kutoa heshima za mwisho
kwa maana hiyo basi taratibu zote za kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea, kwa wakazi wa Dar es salaam na maeneo ya jirani zitafanyika siku ya jumatatuya tarehe 3 / 6 kuanzia saa mbili ya asubuhi mpaka saa sita mchana, ambapo baada ya hapo, safari rasmi ya kuelekea Mororgoro itaanza kwa ajili ya mazishi itaanza.
kamati inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza
0 comments:
Post a Comment