Vodacom
Tanzania na Fenix International zimezindua chaja mpya za simu
'Readysety' zinazotumia nishati ya jua na zenye uwezo wa kuchaji zaidi
ya simu 5 tofauti kwa wakati mmoja kwa minajiri ya kuwawezesha
watanzania hususan waishio maeneo yasiyo na umeme kupata mawasiliano ya
uhakika kupitia simu zao za mikononi.
Mkuu
wa Masoko wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa (kushoto)na mkazi wa
Kibaha Bi Anna Joseph ambaye ni mmoja wa wadau walionufaika na huduma ya
chaja za Readyset,wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani)
namna chaja hizo mpya na zinatumia nishati ya jua zinavyofanya kazi .
Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho hususan
kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia
ubia baina ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Fenix International.
Wanaoshuhudia nyuma ni Meneja wa biashara wa kimataifa wa Fenix
International, Peter Glenn, na Mkurugenzi Mtendaji wa Fenix
International,nchini, Peter Mungoma
0 comments:
Post a Comment