
.
1. Serikali
imesema licha ya kupanga Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutumia
teknolojia ya kisasa katika kuhesabu kura kwenye uchaguzi mkuu ujao,
kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika nchi za Ghana na Kenya
wataweka pia njia mbadala katika kutekeleza zoezi.
Akizungumza
Bungeni wakati wa kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu
MIZENGO PINDA amesema nia ya NEC kuujaribu mfumo huo ni nzuri lakini ili
kuondoa mivutano, Serikali itahakikisha mchakato huo unaendeshwa kwa
matakwa ya wadau wote.
PINDA
ametolea ufafanuzi huo kufuatia swali aliloulizwa na Mkuu wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni FREEMAN MBOWE juu ya kutoaminika kwa mfumo wa
kiteknolojia unaotarajiwa kutumika na tume ya uchaguzi na namna wadau
watakavyoshirikishwa li kujiridhisha nao.
Kivutio
kikubwa kilikuwa ni Mbunge wa Kisesa LUHAGA MPINA ambaye ameonesha
ukomavu wake kisiasa na kuikosoa Serikali kufuatia kushindwa kutekeleza
ahadi zake inazotoa ikiwemo kuwapatia Watanzania wa Vijijini huduma bora
za afya.
2.
Baada ya ukimya wa miaka miwili, Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais
asiye na Wizara maalum Profesa MARK MWANDOSYA ameibuka na kuzungumza
bungeni baada ya kupita kipindi cha miaka miwili na kukemea tabia ya
baadhi ya Wabunge kuzungumzia masuala ya usalama wa taifa hadharani.
Akitumia
fursa hiyo wakati akijibu hoja mbalimbali za Wabunge kuhusiana na
michango katika Bajeti ya Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Profesa
MWANDOSYA amesema usalama wa taifa wako duniani kote hivyo
linapojitokeza tatizo ni vema Wabunge wangejifungia ndani kujadili
kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge.
Kwenye
sentensi nyingine Profesa MWANDOSYA ameshangazwa na kitendo cha
Wabunge kutotoa mchango wowote kuhusiana na masuala ya mipango ya
maendeleo kwa taifa wakati wakichangia hoja kwenye Bajeti ya Ofisi ya
Rais Uhusiano na Uratibu.
3. Mbunge
mwingine wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Kisesa LUHAGA MPINA
amekataa kuunga mkono hoja bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma kwa madai kwamba Serikali imekuwa ikikataa kutekeleza
ahadi inazotoa kwa Wananchi wake.
Amesema
licha ya utekelezaji wa maendeleo kwa jamii nchini kuhitaji kiasi cha
Shilingi Trilioni 16.7 Serikali kupitia Wizara ya Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa TAMISEMI imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 640, mgao
unaoashiria baadhi ya miradi kutofikiwa na fedha hizo.
0 comments:
Post a Comment