P SQUARE:NASISI PIA NI WATU WAKAWAIDA TU

.
.
Mara nyingi waimbaji mastaa wa Nigeria P Square wamekua wakihusishwa na stori za kumiliki ndege yao binafsi na wakati mwingine wamekua wakionekana kutumia usafiri binafsi wa anga kwenda sehemu mbalimbali za Afrika na hata ndani ya nchi yao wanapopata mwaliko wa kufanya show lakini jumamosi iliyopita huko Nigeria Yenagoa, mashabiki wengi waliotarajia P Square wangetumia usafiri wao binafsi wa ndege kwenda kwenye usiku wa African Movie Academy Award walibaki na maswali.
Ilibaki stori tu baada ya mastaa hao kutua na ndege ya kawaida ya abiria tena wakiwa wamejichanganya na abiria wengine (economy) wakiwa na mastaa wengine akiwemo tajiri mwingine mchekeshaji aitwae AY, mwigizaji Chioma Akpotha na wengine wengi.
.
.
Utajiri walionao P Square wakiwa kwenye list ya wasanii watano matajiri Afrika huku wakifanya pia biashara nyinginezo ikiwemo mafuta, ndio unafanya wengi waamini kwamba hawa jamaa wanaishi kistaa zaidi na ni ngumu kujichanganya na abiria kama hivi hasa kwenye safari za karibu ambazo wanaweza kutumia usafiri binafsi.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment