
Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema. Zitto Kabwe
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba
“Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu
mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma
haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu.
Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na
polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na
polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine
yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake
litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya
Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka
zitachukuliwa.
Ushauri- tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation
agents” nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against
provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na
kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini
na ugandamizaji.
0 comments:
Post a Comment