

Habari kutoka Liwale, mkoani Lindi, zinasema kwamba hali si shwari
wilayani humo usiku huu kufuatia fujo kubwa zinazofanywa na wanaodaiwa
kuwa wakulima wa korosho wanaodai malipo yao.
Nyumba nne inasemekana zimeshachomwa moto na ng'ombe kadhaa
wamechinjwa na watu hao. Polisi wameshawasili eneo hilo na mabomu ya
kutoa machozi yameanza kurindima katika harakati za kutawanya watu hao.
Habari hizo zinasema nyumba mbili za Mbunge wa Liwale na Mbili za
mwenyekiti na makamu wa Umoja AMCOS zimechomwa moto, wakati ng'ombe wa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya na za meneja wa Ilulu Union
wamechinjwa.

SUCCI1 Tutaendelea kwuajulisha zaidi kadri habari zitavyotufikia...
0 comments:
Post a Comment