Taarifa za sasa kutoka Arusha
ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anaendelea kushikiliwa na
jeshi la polisi Arusha na kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu za
Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu wa Mkoa Arusha juzi.
Taarifa ya wakili wa Lema,
Humphrey Mtui ni kwamba Mbunge huyu Polisi imekataa kutoa dhamana yake
na kusema mpaka jumatatu ndio itajulikana hatma yake kwenye hii ishu ya
uchochezi.
Mbunge Lema alikamatwa jana saa
tano na nusu usiku na polisi nyumbani kwake ambapo Polisi walimfata,
baada ya kufika kwake walianza kugonga lakini Mbunge huyu alisita
kufungua kwa sababu alizotoa kwamba hakua anafahamu watu wanaogonga
nyumbani kwake usiku, alianza kupigia simu rafiki zake na watu wake
walioanza kukusanyika nje ya nyumba yake.
Muda ulipozidi kwenda polisi
walizidi kukusanyika wakiwa na vifaa na mbwa wao pia kitendo
kilichofanya baadhi ya marafiki wa Lema kumshauri atoke tu nje ambapo
alifanya hivyo na kuchukuliwa mpaka kituoni.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment