Naibu Spika wa Bunge JOB NDUGAI
amemtoa nje ya Bunge kwa muda wa siku tano Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni TUNDU LISSU kwa madai ya utovu wa nidhamu na
kuanzisha majibizano bungeni kitendo kinachokiuka kanuni za bunge.
Wengine ambao wamepewa adhabu
hiyo ya kutohudhuria vikao vya bunge kwa siku tano ni Mbunge wa Mbeya
Mjini JOSEPH MBILINYI, Mbunge wa Arusha Mjini GODBLES LEMA, Mbunge wa
Iringa Mjini Mchungaji PETER MSIGWA, Mbunge wa Nyamagana EZEKIA WENJE na
Mbunge wa Ilemela HIGHNES KIWIA ambao walikuwa wakiwazuia askari wa
bunge kumtoa nje LISSU.
Namkariri Naibu Spika akiongea
nje ya bunge akisema “nimemuonya zaidi ya mara kumi kwa jioni ya leo
peke yake kwamba demokrasia ya kibunge ni ya kuwapa watu wengine nao
nafasi ya kusikika, kila anaesimama anakatishwa yeye kasimama dakika
zake zote amekatizwa na kina nani? kinachokosekana kwenye bunge hili ni
uvumilivu wa kumsikiliza mwingine, watu wanapenda kumshambulia mwingine
lakini hawako tayari kusikiliza wengine wakiwajibu, tunalaumiwa na kila
mtu….. hata hatua nilizozichukua ni hatua ndogo tu”
Kabla ya uamuzi wa kutolewa nje
ya Viwanja vya bunge haujatolewa, Mbunge wa Iramba Magharibi MWIGULU
NCHEMBA ndiye aliyekuwa akichangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma ambapo namkariri hapa akisema “mimi ni
ninachokumbuka labda watu wengine kumbukumbu sijua wanakua na hangover
gani, kitu ninachokitambua kwamba Rais amekua mtu wa kwanza kukemea
jambo la udini, kuna mgombea wa chama kimojawapo alikua anakwenda
anaongea na baadhi ya Viongozi wa kidini kama ndio viongozi na mikutano
ya ndani ya chama chake, hili linakubalika wapi? wakari CCM inatumia
mabalozi, wenyeviti wa tawi…..”
Mbunge wa Longido LEKULE LAIZER
ni kama ametabiri kutokea kwa jambo hilo kabla kwani wakati anachangia
amepinga vitendo vya vurugu bungeni hali iliyopelekea kuwakumbuka
wabunge wa zamani, namkariri akisema “hivi Mbunge mwenzako anapoongea
unaanza kumzomea unafikiria nini? hatujawahi kufikia kiwango hiki”
Sekunde chache kabla ya Naibu
Spika kuagiza Tundu Lissu atolewe, alisema “Mh Tundu Lissu sijui ni huu
ugeni wa kuwa bungeni, ndio lazima nitoe maoni yangu kama kiongozi…
unakuwa wewe ni sehemu ya kufanya vurugu ndani ya bunge? nasema hivi….
askari toa nje Tundu Lissu, askari wakwapi…. toa nje”
Wakati Naibu spika akitoa hilo
agizo, wabunge wengine kadhaa walisikika wakisema…. “haiwezekani…… huo
ni ubabe…. ubabe ubabe…. polisi, tutoke wote…..” unaweza kuwasikiliza
hapa chini..
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment