
.
Zamani
kulikuwa na bia moja ambayo kauli mbiu ya kibiashara ya bia hiyo ilikuwa
maneno “Baada ya kazi ,Burudika” , . Wachezaji wa Manchester United
waliifanyia kazi kauli mbiu hii na kuitendea haki kisawasawa baada ya
kukesha wakila bata kwenye casino na bar za jijila Manchester kufuatia
ushindi wa 3-0 walioupata dhidi ya Aston Villa ambao ulihakikisha
ubingwa kwa klabu hiyo kwa msimu wa 2012/2013.
Wakiongozwa
na kamanda wa bata kwenye kikosi hicho beki Rio Ferdinand , wachezaji wa
United hawakuruhusu uchovu wa mechi uwazuie kula raha na huwezi
kuwalaumu kwani kazi kwa msimu huu imekwisha na wanaruhusiwa kufanya
wanachotaka kwa sasa.

.

.
Hakuna
aliyebaki nyuma kuanzia kwa wachezaji wa kikosi cha pili kama kipa Ben
Amos mpaka kwa mkongwe Ryan Giggs na kipa David De Gea ndio alikuwa mtu
wa mwisho kuondoka club saa 12 asubuhi baada ya usiku wa raha akienjoy
na washkaji zake baada ya kazi ngumu ya msimu huu.
Zifuatazo ni
baadhi ya picha za jinsi hali ilivyokuwa wakati wachezaji wa Man United
walipoliteka jiji la Manchester usiku wa juzi.

.

.

.

.

.



.

.

.

Rio-Ferdinand
alipitiliza na kuondoka bila kumaliza kulipa, hapa ni muhudumu
akimkumbusha kulipa wakati huo Rio alikua ameshaingia kwenye gari
tayari.

Kipa David De Gea ndio alivunja rekodi kabisa kwa kuondoka club saa 12 asubuhi.
0 comments:
Post a Comment