Moja kati ya mabinti waliowahi kuwika katika
muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almas, baada ya kuwa kimya kwa muda,
hatimaye ameibuka na kuweka bayana kuwa ana vitu viwili vikubwa ambavyo
anavifanya kwa ajili ya mashabiki wake.
Katika kufafanua, amesema kwanza, hivi sasa
anaandaa album yake ya 3 kwa sababu mashabiki wake wanauliza sana kuhusu
album mpya, kutokana na maombi yao ameamua aandae.
Mwasiti alisema ingawa album yake iliyopita
iliyoenda kwa jina la 'Kamili' haikumpa mafanikio ya pesa kama
alivyotarajia, lakini atafanya album hiyo kwa ajili ya mashabiki wake na
pia anataka kuifanyia hiyo album tofauti na album zake zilizopita.
Mwasiti, ambaye anashikilia tunzo mbili za muziki
mpaka sasa, huku moja ikiwa kutoka nchi jirani ya Kenya, alieleza
utofauti wa album hiyo nikuwepo kwa aina ya muziki ambao ndo muziki
anaupenda lakini kutokana na soko la muziki ulivyo anashindwa kuufanya.
Katika album yake mpya itakayokuwa na nyimbo 8 atachanganya nyimbo za mahadhi ya Jazz.
Msanii huyo alisema kuwa kwasasa nyimbo ambazo
ziko tayari amefanya katika studio za THT Sound na Ngoma Records, na
hajamshirikisha msanii yeyote.
0 comments:
Post a Comment