Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, Wanawe rais mstaafu wa Afrika Kusini
Nelson Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi wake
watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki.
Makaziwe na Zenani Mandela wanadai kuwa watatu hao hawana haki ya
kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola
milioni 1.1
Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94
Mandela aliondoka hospitalini baada ya kutibiwa ugonjwa wa mapafu
pamoja na homa ya mapafu, na katika rekodi amelazwa hospitalini mara ya
nne katika kipindi cha miaka miwili.
Duru zinasema kuwa kumekuwa na mzozo wa kichinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la Mandela hususan picha alizokuwa anachora akiwa jela.

![]() |
Zenani Mandela |
![]() |
Makaziwe Mandela |
Duru zinasema kuwa kumekuwa na mzozo wa kichinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la Mandela hususan picha alizokuwa anachora akiwa jela.
0 comments:
Post a Comment