BAADHI YA WASANII WALIOKUWEPO MAKABURINI KATIKA KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA WA KIFO CHA MAREHEMU STEVEN KANUMBA


Wasanii mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kaburi la Kanumba.
Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, akiwa na shada la maua pembeni yake ni mama wa marehemu, Flora Mtegoa.
Mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco, akiwaongoza wasanii kutoka Ghana kuweka mashada ya maua juu ya kaburi la Kanumba.
Msanii Yusuf Mlela akiwa na simanzi kaburini kwa Kunumba.
Shabiki mmoja akilia kwa uchungu juu ya kaburi la Kanumba.
Kaburi la marehemu Kanumba lilivyokuwa jana ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kifo chake.
NI mwaka mmoja sasa tangu aliyekuwa mcheza filamu mahiri hapa Bongo, Steven Charles Kanumba, atangulie mbele ya haki. Jana watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa ndani na nje ya nchi waliungana kwa ajili ya kumbukumbu za staa huyo.
Kumbukumbu hizo zilianzia katika Kanisa Kuu la Kilutheli Tanzania (KKKT), lililopo Kimara Temboni na baada ya hapo masafara ulielekea katika makaburi ya Kinondoni alipozikwa msanii huyo kwa ajili ya sala fupi na kuweka mashada ya maua. Shughuli hizo zilihitimishwa katika Viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuangalia filamu yake ya mwisho aliyocheza inayoitwa Power and Love.
(PICHA : GLADNESS MALLYA NA IMELDA MTEMA / GPL)
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment