Dar. Miaka mitatu imepita tangu
CD ya wimbo wa taifa ilipogoma kwenye Uwanja Taifa mbele ya Rais Jakaya
Kikwete wakati wa mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Morocco.
Sakata la kugoma kwa wimbo wa taifa lilifunika kipigo cha bao 1-0 ilichopata Stars kutoka kwa Morocco, pia Serikali iliagiza matumizi ya ‘brass band’ kwa ajili ya kupigwa nyimbo za taifa kila inapocheza Taifa Stars.
Sakata la kugoma kwa wimbo wa taifa lilifunika kipigo cha bao 1-0 ilichopata Stars kutoka kwa Morocco, pia Serikali iliagiza matumizi ya ‘brass band’ kwa ajili ya kupigwa nyimbo za taifa kila inapocheza Taifa Stars.
Leo Taifa Stars inashuka kwenye uwanja huo kuivaa
Morocco katika harakati zake za kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki
Fainali za Kombe la Dunia 2014.
Kikosi cha Kim Poulsen kimeonyesha mabadiliko
makubwa katika kipindi cha mwaka mmoja kikiwa na rekodi za kuwafunga
mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia na Cameroon zote zilifungwa bao
1-0.
Kocha wa Stars, Kim ni dhahiri ataingia uwanjani
huku akiwa na matumaini makubwa ya kuwadhoofisha wapinzani wake na
kupata ushindi kwani tayari alishaisoma Morocco na kujua ubora na
udhaifu ilionao ilipokuwa inashiriki katika Fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika zilizofanyika nchini Afrika Kusini mapema mwaka huu.
“Nimeiona Morocco katika mechi tatu tofauti kule
Afrika Kusini ilipokuwa inashiriki michuano ya Kombe la Afrika. Ni timu
nzuri na ina wachezaji wanaocheza soka katika klabu kubwa barani Ulaya,
kimsingi nguvu yao ipo katika uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, lakini sisi
tutacheza kwa umoja zaidi na kuhakikisha tunashinda mchezo wa
leo,”alisema Kim.
Naye mshambuliaji Mbwana Samata wa Taifa Stars
anaingia kwenye mchezo wa leo akiwa na rekodi nzuri baada ya kuiongoza
TP Mazembe kupata ushindi dhidi ya Mochudi nchini Botswana. Pia macho ya
mashabiki wengi yatakuwa katikati ya uwanja wakati Abubakari Salum
‘Sure Boy’ na Frank Domayo watapokuwa wakionyesha ufundi wa kugawa pasi
fupi na ndefu.
Kikosi: Juma Kaseja, Erasto
Nyoni, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Agrrey Morris, Frank Domayo, Amri
Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngasa, Mbwana Samata na Salum Abubakar.
0 comments:
Post a Comment