Mwimbaji
Linah ambae juzi alitangaza kwamba ameamua kuwazawadia wazazi wake
nyumba aliyoijenga Mpiji Mbezi Dar es salaam kwa thamani ya milioni 30
za kitanzania, amesema pamoja na wazazi wake kufahamu kwamba matunda
hayo yametokana na muziki peke yake, amekubali kwamba baba yake mzazi
mpaka sasa bado hakubaliani na mavazi anayoyavaa Linah.

Namkariri
Linah akisema “nimejitahidi sana kuwaelezea wazazi wangu wanielewe
litakapotokea tatizo lolote itakua ni bahati mbaya tu lakini sio kwa
makusudi, baba anaona pia kwenye magazeti huwa navaa hivi najitahidi
kumwambia hivyo ni vitu vya bahati mbaya huwa vinatokea na mimi kama
msanii ndio maana tunakula tunaishi lakini ndio kazi”
Mbali
na hayo Linah kasema “nyimbo zangu baba anazisikiliza na anazipenda na
anakubali ninaimba kitu ambacho kipo, ila ubishi mkubwa kati yangu na
yeye ni mavazi, kuna show na show.. siwezi kwenda kufanya show ufukweni
alafu nimevaa magauni, show nyingine tunatakiwa kubang siwezi kuvaa
migauni kama niko kanisani”
0 comments:
Post a Comment