SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo lilisimamisha
mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kutokana na baadhi ya wagombea kulalamika kuenguliwa sasa litatuma
ujumbe wake nchini katikati ya mwezi ujao.
Ujumbe huo ambao
moja ya shughuli zake kuwasikiliza wote walioenguliwa na Kamati ya
Rufani ya Uchaguzi ya TFF na hawakuridhika na uamuzi huo, utakuwepo
nchini Aprili 16 na 17 mwaka huu.
Kwa mujibu wa barua ya
Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar
Tenga, kazi ya ujumbe huo ni kubaini tatizo lililopo na kutoa ripoti kwa
mamlaka zinazohusika ndani ya FIFA kwa ajili ya kutoa mwongozo.
Ujumbe
huo utakutana na pande mbalimbali zinazohusika wakiwemo wagombea,
kamati za uchaguzi za TFF. Lakini pia ujumbe huo unatarajia kumtembelea
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara
pamoja na watendaji wake wizarani.
Uchaguzi wa viongozi wa TFF ulikuwa ufanyike Februari 24 mwaka huu,
lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa
kulalamika kuwa hawakutendewa haki na wangependa shirikisho hilo
liingilie kati.
Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.
0 comments:
Post a Comment