Wakati wafuasi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) wakipanga kufanya maandamano makubwa leo jijini Dar
es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya kushinikiza Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ajiuzulu, Jeshi la Polisi
limewapiga marufuku kwa maelezo kuwa maandamano hayo ni batili.
Takriban wiki mbili zilizopita viongozi wa chama
hicho katika mikoa hiyo, kwa nyakati tofauti walitangaza kufanyika kwa
maandamano hayo, lengo likiwa ni kushinikiza Dk Kawambwa na naibu wake,
Philipo Mulugo kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya watahiniwa wa
Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana.
Wakati polisi wakizuia maandamano hayo kwa maelezo
kuwa Serikali imeshaunda tume inayoongozwa na Profesa Sifuni Mchome,
kuchunguza chanzo cha kufeli kwa asilimia 65 kwa watahiniwa hao, Chadema
wamesema lazima maandamano yafanyike na wako tayari kufa.
Kauli ya Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesisitiza kuwa maandamano ya kumshinikiza Dk Kawambwa kujiuzulu yatafanyika kesho kama yalivyopangwa licha ya Jeshi la Polisi kuyapiga marufuku.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesisitiza kuwa maandamano ya kumshinikiza Dk Kawambwa kujiuzulu yatafanyika kesho kama yalivyopangwa licha ya Jeshi la Polisi kuyapiga marufuku.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mbowe alisema
iwapo Serikali itaamua kutumia risasi na mabomu kuua raia wake
wanaoandamana kwa amani kuonyesha hisia ya kuchukizwa na matokeo mabaya
ya kidato cha nne, basi itimize dhamira hiyo kwa kuwapiga risasi
waandamanaji.
“Kama CCM na serikali yake itatumia risasi na
mabomu kuua watu kumlinda waziri mmoja asijiuzulu, basi wafanye hivyo.
Sisi tutaandamana kama tulivyotangaza mwezi mmoja uliopita na tunaomba
dunia ielewe hivyo,” alisema Mbowe.
Alisema wameamua kuendelea na maandamano hayo
baada ya kutoridhishwa na sababu zilizotolewa na polisi kuzuia
maandamano hayo, ikiwamo ile ya CCM kudaiwa kuandaa maandamano siku
hiyohiyo kupitia njia zilezile zilizotajwa na Chadema.
Mbowe alisema maandamano hayo yatafanyika katika
majiji manne ya Arusha, Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam na kuwataka
wananchi wanaoishi jirani na miji hiyo kujitokeza kwa wingi kuandamana
kwa mustakabali wa watoto wao wasiopata elimu bora kama wapatayo wale wa
viongozi.
Chadema Mkoa wa Dar
Katibu wa Chadema Kanda ya Dar es Salaam, Henry Chilewo akizungumza na vyombo vya habari jana alisema, maandamano hayo yatahusisha wananchi wa kada zote.
“Mwenyekiti wetu (Freeman Mbowe) alitoa siku 14 kwa viongozi hao wajiuzulu kwa hiyari lakini wamegoma, tunaamini nguvu ya umma wa Watanzania itafanikisha hilo na ifahamike wazi kuwa lengo letu ni kudai elimu bora kwa watoto wetu,” alieleza Chilewo.

Kauli ya Kamanda Kova
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliliambia gazeti hili kwamba bado jeshi hilo linafanya tathmini kabla ya kutoa kauli ya mwisho.
“Bado tunafanya tathmini, kesho (leo) tutaeleza kama yatakuwapo au hayatakuwapo,” alisema Kova.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, Englebert Kiondo alisema maandamano hayo ni batili kwa sababu tume imeshaundwa.
“Kesho (leo) Rais wa China, Xi Jingping anakuja
nchini hivyo si vizuri akafika na kukutana na maandamano, nawaomba
wananchi wa Temeke wasishiriki katika maandamano haya, waendelee na
shughuli nyingine,” alisema Kiondo.
0 comments:
Post a Comment