AT AKANUSHA UVUMI ULIO SAMBAA KWA WATU

AT
Msanii kutoka Tanzania Mwenye mashabiki wengi Mombasa alikuwa kwenye michakato ya Kufanya Video Yake Mpya Weekend iliyopita na Video hii ilibidi ifanyike Mombasa. Baada ya Shooting ya video hii kukamilika AT Alikuwa tayari kurudi Dar es salaam kwani alikuwa na Show ya Jumapili Ndani Ya Club Bills. Japokuwa alikuwa na majukumu Dar es salaam, alipata nafasi yakufanya show kwenye jukwa la mmoja ya wagombea wa Ugavana pale Mombasa na Mgombea huyu anakubalika sana Mombasa Ndio maana Ilikuwa Rahisi kwa AT Kukubali kufanya Show yake.
Story kutoka Mombasa zinasema kuwa AT Alipigwa na kushushwa Kwenye Jukwa kabla show hio kuisha, AT Amefunguka leo kupitia sammisago.com kuwa story hizi ni za uongo na anakanusha taarifa hizi kabisa na hakuna kitu kama hicho. AT Amekaririwa na sammisago.com akisema show hio imefanyika na kuisha vizuri. Mgombea aliye fanya show yake anakubalika sana na hakuna mtu aliye leta fujo kwenye show hio. Pia AT Amesema kilicho mchelewesha Dar es salaam ni kuchelewa kufika Airport ndio ikabidi atumie gari mpaka Tanga na kuonganisha mpaka Dar es salaam.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment