BEAUTIFUL
Onyinye, Wema Isaac Sepetu kama kawa ameshuka na mpya ya kumpulizia
mbwa wake pafyumu yenye thamani ya dola 120 (zaidi ya shilingi
180,000).Mkali huyo asiyekaukiwa na matukio Bongo amefunguka kuwa
analazimika kumgharamia mbwa huyo pafyumu hiyo kwani ni moja kati ya
viumbe ambavyo anavihusudu kupita maelezo.
“Lazima
anukie kama mimi ninavyonukia, pafyumu humfanya anukie vizuri hata
ninapokuwa nimetoka naye mitaani naye anaonekana kweli ni mbwa wa staa,”
alisema Wema.
Kuhusu manunuzi, mkali huyo anayekimbiza kwenye soko
la filamu Bongo alisema mara nyingi pafyumu hizo huwa anaagiza kutoka
nje au kwa watu wake maalum hapa Bongo ili kuwa na utofauti wa ubora na
hadhi yake ya kistaa.
Wema aliendelea kusisitiza kuwa mbwa huyo huwa anampa kampani na
wakati mwingine humfurahisha pindi anapokuwa ameboreka au anapokuwa peke
yake nyumbani.
“Mara nyingi huwa naagiza kutoka Uarabuni, unajua kule pafyumu zao ni nzuri na ubora wake ni wa hali ya juu,” alisema Wema.
Mkali huyo mara nyingi amekuwa akitumia pafyumu za kuanzia dola 300 (shilingi laki nne na nusu) na kuendelea.
Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.
0 comments:
Post a Comment