
Padre huyo alikuwa akitoka katikati ya mji kwenda
eneo la Mtoni Bububu kwa ajili ya kuendesha misa katika Kigango
kilichopo eneo hilo, ndipo mauaji yakamkuta akiwa anaingia tu eneo la
kanisa.
Tukio hilo la kinyama lilitekelezwa na watu
wasiojulikana limeendeleza hofu katika visiwa hivi hasa ikizingatiwa
kuwa mwezi Desemba mwaka jana, watu kama hao wakiwa na pikipiki aina ya
Vespa walimshambulia kwa risasi Padre Ambrose Mkenda, hali inayoonyesha
kuna mkakati wa kushambulia viongozi wa dini visiwani humo.
Tukio jingine ni lile la kumwagiwa tindikali kwa kiongozi wa Kiislamu, Sheikh Fadhil Soraga ambalo pia lilitokea mwaka jana.
Matukio kama haya yanaendelea kushika kasi na
kuzua hofu kwa viongozi wa dini huku kila mmoja akijiuliza zamu yake
itakuwa lini, hasa ikizingatiwa kuwa Jeshi la Polisi licha ya kuunda
vikosi na kuweka mikakati limeshindwa kuwatia nguvuni wanaotekeleza
mashambulizi hayo.
Mapema mwaka jana baada ya kujitokeza kwa makundi
yanayopinga Muungano yakiongozwa na kundi la Uamsho linalohusisha
jumuiya za dini ya Kiislamu, yaliishia na vurugu zilizosababisha
makanisa kadhaa kuchomwa moto na kuharibiwa kwa mali za makanisa hayo.
Kwa kifupi, hali ya amani Zanzibar inatia shaka huku udini ukiwa unashika kasi.
Hali hiyo pia imebisha hodi upande wa Bara ambapo vurugu zimezuka katika maeneo mbalimbali.
Hivi karibuni tumeshuhudia machafuko mkoani Geita
zilizosababisha kifo cha mchungaji mmoja na watu wengine 10 kujeruhiwa
baada ya Wakristo kufungua bucha yao, hali iliyowaudhi Waislamu na
kuivamia.
Suala la kuchinja wanyama nalo sasa limechukua
hatua mpya baada ya Wakristo nchini hasa Kanda ya Ziwa kudai haki yao ya
kuchinja kama wanavyofanya Waislamu.
Katika kujaribu kutatua suala hilo, Waziri Nchi
katika Ofisi ya Rais Sera na Uratibu Stephen Wassira na Waziri Mkuu
Mizengo Pinda wamekaririwa wakitaka utaratibu wa Waislamu kuchinja
wanyama katika machinjio ya umma uendelee ili kuepusha shari.
Nadhazni suala hili linapaswa kujadiliwa na pande hizo mbili kwa kina ili kutafuta suluhu ya kudumu.
0 comments:
Post a Comment