Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa pesa hizo
katika makao makuu ya ofisi za kampuni hiyo yaliyoko Mlimani City jijini
Dar es Salaam, Bi, Ruth John Mungule Mkazi wa Kimara jijini Dar es
Salaam amesema kuwa anaamini asinge kuwa mtoto wake kutumia ujanja
kushiriki mchezo huo asinge weza kushinda pesa hiyo.
“Siku ya jumatatu asbui wiki iliyopita mtoto wangu aliniomba kutuma
message ili kushiriki hii Vodacom MAHELA, nilimruhusu siku iliyofuata
juma nne nilipigiwa simu kutoka Vodacom kuambiwa kuwa nimeshinda
shilingi Milioni moja, haikuwa rahisi kuamini lakini hadi leo nimefika
hapa na kukabidhiwa fedha zangu nimeamini ni kweli.
Mshindi mwingine alieshinda katika droo iliyo chezeshwa jana (jumatatu)
ambaye ni askari polisi, Bi Liberata Karigita Mkazi wa Kilwa Road Balax,
jijini Dar es Salaam, katika mahojiano yake kwa njia ya simu na Meneja
wa mawasiliano wa Vodacom wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya pili
alisema kuwa muda mwingi alipokuwa akiwasihi wenzake kushiriki
walimcheka na kumbedha.
“Mara nyingi nilipokuwa nashiriki kwa kutuma message Askari wenzangu
walinicheka na wengine kunibeza kuwa napoteza fedha zangu bure lakini
leo Vodacom wamenitoa aibu na nimwshinda milioni tano nashukuru sana
Vodacom, alibainisha Askari huyo.
“Tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuitikia wito wetu na kushiriki
vizuri katika promosheni yetu hii ya VODACOM MAHELA, Ninawasihi wateja
wengine hata ambao hawajajiunga na Vodacomm kuhakikisha wanajiunga na
kushiriki katika promosheni hii, MAHELA, ni kwa watanzania wote, alisema
Rukia Mtingwa, Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania.Hadi kufikia sasa
tayari kampuni ya Vodacom kupitia promosheni yake ya Vodacom Mahela
imepata jumla ya washindi 31 ambapo mshindi wa jumla atajishindia
milioni 100 katika droo kubwa itakayo chezeshwa baada ya siku tisini za
muda wa promosheni hiyo.
0 comments:
Post a Comment