
STAA wa filamu za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa tangu
Elizabeth Michael ‘Lulu’ atolewe gerezani kwa dhamana, moyo wake unakuwa
mzito kukutana naye.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Maya aliweka plain kuwa kila
anapofikiria ukaribu aliokuwa nao na marehemu Steven Kanumba, moyo wake
unakuwa mzito kumuona Lulu ambaye alikuwa mpenzi wa marehemu.
“Mh! Kukutana na Lulu ni ngumu sana, sijui hata najisikiaje? Moyo
unakuwa mzito sana kukutana naye na sijui kwa nini,” alisema Maya.
0 comments:
Post a Comment