KWA WAKE ZA WATU... YAJUE MADHARA YA KUENDEKEZA UTANI KWA WANAUME WAKWARE!


NI matumaini yangu kuwa umzima buheri wa afya na unaendelea vyema na mishemishe zako za kimaisha.
Mimi nipo poa tayari kukuletea mada ambayo naamini itakuwa ni yenye faida kubwa kwako.
Mpenzi msomaji wangu, unapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi au ndoa, yapo mambo madogomadogo ambayo ukiyapa nafasi kuna uwezekano mkubwa ukaharibu vitu flani.
Mambo hayo yapo mengi lakini leo nataka kuzungumzia hii tabia ya baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa au wana wapenzi wao kupenda sana kutaniana na wanaume.
Nimelazimika kuzungumzia hili kwa kuwa nimebaini wengi wameachika na wengine wako kwenye uhusiano usiyo na maelewano kufuatia tabia yao ya kupenda kutanianataniana na wanaume tena kwa mambo ya kijinga.
Sikatai, utani si kitu kibaya kwani hata kwenye somo la Kiswahili kwa wale wenzangu tuliopitia huko tunaambiwa kuwa, utani unaongeza uhusiano mzuri baina ya mtu na mtu lakini pia unaleta furaha.
Ila sasa utani ninaotaka kuuzungumzia hapa ni ule uliopitiliza. Hivi karibuni nilipata fursa ya kusuluhisha mgogoro wa kindoa uliokuwepo kati ya rafiki yangu na mkewe.
Chanzo cha mgogoro huo ilikuwa ni sms ambayo mwanaume aliibamba kwenye simu ya mkewe ikitoka kwa kijana ambaye ni maarufu sana pale mtaani kwao.
Meseji yenye uliandikwa hivi: ‘Umejaaliwa kweli, yaani mumeo anafaidi sana.’ Baada ya kijana huyo kumtumia mke wa mtu huyo sms hiyo, bila hiyana yule mke wa mtu akajibu: Mh!Una mambo wewe, au na wewe unataka?”
Kuchati huko ndiko kulikomfanya rafiki yangu kuona mkewe amejiachia sana kwa kijana huyo kiasi cha kufikia hatua ya kuambiana maneno hayo. Cha ajabu mke wa mtu huyo alijitetea kuwa walikuwa wakitaniana tu.
Hivi inakuwaje mke wa mtu unakubali kutaniwa kirahisi na wewe unaonekana kufurahia tu? Ni utani gani huo wa kusifiana maumbile au kushikwashikwa kisha unachukulia poa?
Kama ulikuwa hujui, wanaume wengi wanapotaka utani na mke wa mtu, wanatengeneza mazingira ya kutongoza na wachunguzi wanaeleza kuwa, mke wa mtu anapotongozwa na mtu ambaye wamekuwa wakitaniana sana tena ule utani wa kijinga, ni vigumu kuchomoa.
Sasa kwa nini uiweke ndoa yako rehani kwa kuweka mbele utani wa kijinga? Kwa nini usiiheshimu ndoa yako kwa kujiweka mbali na wanaume ambao wanaweza kuibomoa ndoa yako?
Wanawake wengine ni wa ajabu sana. Unamkuta anajenga ukaribu na baadhi ya wanaume na kufikia hatua ya kutaniana nao katika mambo ambayo mwishowe huwa kutongozana.
Mwanamke aliyeolewa au mwenye mpenzi wake hatakiwi kujenga ukaribu na wanaume wa pembeni. Cha msingi ni kuwaheshimu na kutowachukulia kuwa ni maadui.
Unapopita maskani wamekaa wavulana, wasalimie kisha chukua hamsini zako, utani wa kijinga epukana nao kwani mwisho watakutongoza na ukionesha kuchukia watadai walikuwa wanakutania kumbe wako ‘sirias’.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment