Ikiwa ni siku chache zimepita
tangu kuuwawa kwa risasi kwa padre Evarist Mushi huko Zanzibar, watu
wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadae kulichoma moto kanisa
la Walokole la Shaloom lililoko Kiyanga kwa Sheha mkoa wa kusini Unguja
Zanzibar.
Kamanda wa polisi mkoa wa
kusini Unguja Agustino Ulomi amesema hilo tukio limetokea jana saa tisa
na nusu usiku, ambapo huo moto ulianza kuwaka baada ya vijana watatu
walioonekana karibu na kanisa, baadae kidogo ndio mlinzi akaanza kusikia
mawe yakirushwa juu ya bati.
Baada ya mlinzi kuona hatari
ilibidi akajifiche lakini kwa mbali akawa anaona kinachoendelea, moto
ukiendelea ndio akampigia simu kiongozi wa kanisa ambae aliwapigia
polisi, wakaja wakawa wanashirikiana na wananchi kuuzima japo tayari
ulikua umeshaunguza samani mbalimbali za kanisa hilo, kilichosaidia
kanisa hilo kutoungua lote ni vifaa imara vilivyotumika kulijenga.
Katika ripoti hii ambayo
imeripotiwa na mwandishi wa habari Cathbert Kajuna wa
kajunason.blogspot.com bado hajakamatwa mtu yeyote mpaka sasa, polisi
wamesema pia wanaanza utaratibu wa ulinzi wa makanisa kutokana na
vitisho vilivyopo sasa hivi.
Nimeongea na mwandishi wa
habari wa millardayo.com kutoka Zanzibar jioni hii, kasema hakuna mtu
yeyote aliejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea saa tisa usiku wa
kuamikia leo, endelea
kuwa karibu naSucci1.blogspot.com na twitter.com/@sundaysucci ambapo utakua wa kwanza
kufahamu pale tu taarifa zitaponifikia.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment