Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na maafisa mbalimbali wa ubalozi wa
Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole
jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria
hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na
Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete,
kabla ya kurejea Dar es salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi
ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta,
aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake
Balozi wa
Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa
ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege
yake ikiondoka uwanjani hapo leo jioni ya Februari 24, 2013.Picha na
IKULU
0 comments:
Post a Comment